Thursday , 12th Jun , 2014

Polisi mkoa wa Pwani nchini Tanzania, inawashikilia watu watano, kwa tuhuma za kuhusika katika tukio ambapo watu wasiofahamika walivamia kituo kidogo cha polisi cha Mkamba Wilayani Mkuranga na kumuua askari polisi mmoja, kujeruhi na kuiba bunduki 5.

Mkuu wa polisi nchini IGP Ernest Mangu.

Mkuu wa polisi mkoa wa Pwani Kamanda Basilio Matei amesema hayo leo katika mahojiano na East Africa Radio wakati akiwa katika maandalizi ya kuusafirisha mwili wa askari aliyeuawa Kopro Joseph Ngonyani kwa ajili ya kuusafirisha kwa mazishi nyumbani kwao mkoa wa Ruvuma.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, watu hao wamekamatwa na kikosi kazi kilichoundwa na makao makuu ya polisi, ambacho amesema kinatumia weledi mkubwa katika kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa pamoja na kurejeshwa kwa silaha zote zilizoibiwa wakati wa tukio hilo.