Tanzania U-15 yaanza kwa sare Botswana
Tanzania imeanza Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) inayofanyika nchini Botswana kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Mali kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 katika mechi iliyochezwa leo (Mei 22 mwaka huu).