Sikika yataka bajeti wizara ya afya iongezwe
Utafiti wa shirika lisilo la kiserikali la Sikika nchini Tanzania unaonyesha kwamba zaidi ya vituo elfu 5 vinavyotoa huduma ya afya kwa umma, havina dawa muhimu na hivyo kusababisha wananchi wanaofika katika vituo hivyo kukosa huduma.