Mgombea urais hatakiwi kuwa na Doa- Jaji Ramadhani
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayewania kuteuliwa na chama chake katika nafasi ya Urais, Jaji Augustino Ramadhani ametaja sifa za mtu anayefaa kuwa Rais wa Tanzania kuwa ni pamoja na kuwa muadilifu na asiyekuwa na doa lolote.
