Azam FC na Mwadui kukutana leo mechi ya kirafiki
Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC kesho usiku watamenyana na wageni wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

