Kala: Tuwapime wagombea kwanza
Katika muendelezo wa upepo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, msanii na mwanaharakati Kala Jeremiah, ametoa angalizo kwa watanzania kutokufuata kundi la watu kufanya uchaguzi wao, bali wasimame kupima uwezo wa viongozi husika.