Twiga Stars kuweka kambi Visiwani Zanzibar
Timu ya Soka ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini hii leo kisiwani Zanzibar kujiandaa na Fainali za Michezo ya All Africa Games zitakazofayika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzavile.