Serikali kuangalia upya aina ya Uwekezaji nchini
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema wakati Tanzania inajiandaa kutekeleza awamu ya pili ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016 -2020) ambao unalenga kukuza viwanda nchini, haina budi kuangalia ni aina gani ya uwekezaji unafaa kuchukuliwa.

