Lema atangazwa mshindi Jimbo la Arusha Mjini
Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.