Wachumi wapongeza sheria mpya ya manunuzi ya umma
Baada ya serikali kuwasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma ambao umelenga kuziba mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha, baadhi ya wanataaluma wa masuala ya uchumi wamesema lengo la sheria hilo ni jambo zuri.