Urasimashaji wa ardhi kutatatua migogoro Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, amesema kuwa mradi wa upimaji na kuwezesha wananchi kupata ardhi utasaidia kutatua kwa kiasi kikubwa cha migogoro ya ardhi mkoani humo na kuufanya mkoa kuendelea kuwa ghala la taifa la chakula.