Kocha Bafana Bafana asimamishwa kwa kumtusi Rais
Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), limemsimamisha Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya nchini hiyo, maarufu kama Bafana Bafana, Ephraim ‘Shakes’ Mashaba, masaa 24 tu baada ya kuiongoza timu hiyo kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal.