Hakuna mashindano yatakayovuruga ligi kuu - TFF
Shirikisho la Soka nchini TFF limesema, hakuna michuano yoyote mipya waliyoianzisha itakayoweza kubadili ratiba ya mzunguko wa pili wa michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo itaendelea Desemba 17 mwaka huu.