Alfred Lucas
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, michuano iliyopo kwa hivi sasa ni ileile ya siku zote ambayo ni ligi kuu yenyewe, kombe la shirikisho, ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, ligi ya wanawake, Ligi daraja la kwanza na la pili na wanaamini hakutakuwa na mabadiliko ya aina yoyote.
Amesema wanajitahidi katika ratiba ya mzunguko wa pili kuweza kuifuata kama ilivyopangwa ili kuepukana na malalamiko kutoka kwa vilabu mbalimbali shiriki vya ligi kuu hapa nchini.





