Wananchi waitwika mzigo Ofisi ya Takwimu
Ikiwa ni siku moja tangu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo kutangaza kushuka kwa mfumuko wa bei nchini wafanyabiashara na wananchi wamekuwa na mitazamo tofauti huku wakidai kuwa takwimu haziakisi maisha ya mwananchi wa kawaida.