Kamera zamuumbua shabiki mtukutu wa Arsenal
Klabu ya soka ya Arsenal imethibitisha kuwa kwa msaada wa kamera za usalama 'CCTV Camera' katika uwanja wa Emirates, wamefanikiwa kumbaini shabiki ambaye alimpiga na chupa ya maji kichwani mchezaji Dele Alli wa klabu ya Tottenham.