Membe, Makamba na Kinana waitwa kuhojiwa CCM
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na Watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Mwanza chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.