Serikali kukarabati Vyuo vyote vya Kilimo
Serikali imeeleza dhamira yake ya kukarabati vyuo vyote vya kilimo nchini ili kukabiliana na changamoto zinazovikabili vyuo hivyo ambapo ni pamoja na uchache na uchakavu wa vitendea kazi kama maabara, vifaa vya TEHAMA, na zana za kilimo yakiwemo matrekta.