CHADEMA yakaribisha hata ambao hawakutia nia
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, ametoa rai kwa wanachama wote wa chama hicho, hata wale ambao hawakutia nia za kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo Urais, wajitokeze kwa ajili ya kwenda kuchukua fomu za kuwania uteuzi ndani ya chama.

