Namungo haiwezi kuwa kama KMC au Singida Utd.
Uongozi wa klabu ya soka ya Namungo Fc, umesema licha ya wao kuwa huu ndio msimu wao wa kwanza ligi kuu,hawapendi kuona wanalinganishwa na vilabu vya KMC na Singida United ambavyo katika msimu wao wa kwanza kama wao walionyesha uhai lakini misimu iliyofuata timu hizo zimeyumba.

