Ijue sababu ya ACT kutohudhuria uzinduzi wa jengo
Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Janeth Rithe, amesema kuwa hawakuhudhuria shughuli ya uzinduzi wa jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapo jana Jijini Dodoma kwa kuwa wako Mikoa ya Kusini wakiendelea na shughuli za kuimarisha chama kuelekea Uchaguzi Mkuu.

