Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa Chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe.
Janeth ametoa kauli hiyo leo Julai 23, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio na kuongeza kuwa CCM kwa kipindi chote imekuwa ikifanya siasa, hivyo na wao ni zamu yao kuifidia miaka zaidi ya minne ambayo walikaa bila kufanya siasa.
"Viongozi karibu wote tuko kusini mwa Tanzania kwenye ziara za kuratibu namna ya kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu. hivyo inawezekana kabisa mwaliko uko ofisini lakini sisi hatukuweza kuhudhuria ni kitu cha kawaida uzinduzi wa jengo ni kama harusi ambapo mtu unaweza kuchanga na mwisho wa siku usiweze kuhudhuria", amesema Janeth Rithe.
Jana Julai 22, 2020, Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini, lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.






