Tuesday , 7th Apr , 2015

Ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea kutimua vumbi hapo kesho katika viwanja viwili jijini Dar es salaam.

Vinara wa ligi hiyo Yanga SC wanatarajia kuwakaribisha Coastal Union kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo Yanga wanaongoza msimamo kwa kuwa na Pointi 40 huku Coastal ikiwa nafasi ya saba kwa kuwa na Pointi 24.

Uwanja wa Chamazi, wenyeji timu ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kuwa na Pointi 36, watawakaribisha timu ya Mbeya City FC yenye Pointi 24 pia ikiwa nafasi ya nane.