
Hii inatokea kwa sababu watu wamekuwa na uhuru kwenye mitandao ya kijamii kuandika na kuweka taarifa ambazo kwa kiasi kikubwa hawana uhakika nazo.
Kampuni ya META inayomilikiwa na Bilionea Mark Zuckerberg imepanga kuja na kitu kipya ambacho kinafahamika kama ''Community notes'' kwenye mitandao yao (Facebook, Instagram na Threads)
Community notes kuielezea kwa lugha nyepesi ni feature ambayo inamsaidia mtumiaji wa mtandao husika kuweka ukweli kuhusu chapisho husika ikiwa taarifa zilizowekwa au chapisho husika halina uhalisia.
Community Notes si ngeni, kupitia mtandao wa X ilitambulishwa mwaka 2022 ikiwa na lengo kuu la kuondoa uvumi wa uongo kuhusu Uviko-19 na baadae vita ya Ukraine na Russia kwenye mtandao huo ambao zamani ulikuwa ukifahamika kama Twitter.
Kuletwa kwa huduma hii kwenye mitandao ya META inaenda kuwa msaada mkubwa sana kwani itasaidia kupunguza taarifa za uongo kwenye mtandao huo, na kwa kuanza itakuwa ni tarehe 18 mwezi huu kwa watumiaji wa mitandao hii nchini Marekani na baada ya hapo kusambaa kwa watumiaji wa mataifa mengine.