Wednesday , 12th Mar , 2025

Kiungo wa Yanga SC Stephane Aziz Ki na mlinzi wa Simba SC Valentino Nouma wameachwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichoitwa leo na kocha Brama Traore kwaajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026

Aziz Ki and Valentine Nouma

Burkina Faso itakuwa nyumbani Machi 16 2025 kucheza mchezo wake wa 5 wa hatua ya makundi dhidi ya Djibouti kabla ya kusafiri kuwafuata Guinea Bissau tarehe 23 Machi 2025

Ikumbukwe kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwepo katika kikosi kilichocheza mechi za mwanzoni za michuano hiyo akicheza michezo mitatu na kutoa pasi moja ya goli

The Stallions wanashika nafasi ya 3 katika kundi A ikivuna alama 5 katika michezo minne iliyocheza, nyuma ya Guinea Bissau yenye alama 6 na Misri mwenye alama 10 anayeongoza msimamo wa kundi hilo