Wednesday , 5th Mar , 2025

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ametoa onyo kwa Man United kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England Jumapili Machi 09/2025.

Mikel Arteta - Kocha wa Arsenal

Maneno hayo ameyasema baada ya timu yake kuisambaratisha PSV Eindhoven kwa magoli 7-1 Jumanne usiku kwenye mchezo wa UEFA.

The Gunners walikuwa hawajafunga goli katika mechi zao mbili mfululizo zilizopita kabla ya kukutana dhidi ya PSV Eindhoven, ushindi wa goli 7 ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea ugenini kwa klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Ulikuwa usiku wa kipekee, ni wazi imetupa furaha na imani nyingi si leo tu, hata kile tutakachofanya kesho. Tunaenda Old Trafford jinsi tunavyocheza tunaweza kushinda mchezo. tumestahili ushindi dhidi ya PSV, nimelichukua hilo na tutaendelea kuimarika kama timu."-Mikel Arteta