
LeBron James
Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 40 alifikisha alama hizo mapema katika robo ya kwanza ya ushindi wa 136-115 wa timu yake, akifunga point 3 kwa kuzamisha mpira wa futi 25 akipokea pasi kutoka kwa Luka Doncic.
James mfungaji bora katika historia ya NBA alimaliza mechi akiwa na pointi 34 na kufikisha jumla ya pointi 50,033 katika maisha yake ya basketball akiwa na alama 6,000 mbele ya Kareem Abdul-Jabbar anashika nafasi ya pili.
"Nimebarikiwa sana kuweza kuweka alama nyingi katika kazi yangu kwenye ligi bora na dhidi ya wachezaji bora zaidi ulimwenguni ." LeBron baada ya kufikia rekodi hiyo katika msimu wake wa 22 wa NBA