Jumatatu , 3rd Mar , 2025

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Luke Pollard amesema kuwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya Ufaransa na Uingereza kuhusu pendekezo la usitishaji mapigano Ukraine

Alipoulizwa kuhusu mpango huo, ambao Macron alieleza gazeti la Ufaransa Jumapili, Luke Pollard alisema Huu sio mpango tunaoutambua kwa sasa.

Anasema kuwa mapendekezo kadhaa yanajadiliwa kwa faragha.

Pollard anasema kilicho muhimu ni kutengeneza mpango utakaoleta amani ya kudumu haraka iwezekanavyo.

Amesema kuwa Marekani ni mshirika muhimu na itaiunga mkono Uingereza, akitaja uhusiano wa kina wa ulinzi kati ya nchi hizo mbili.

Haya yanajiri baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, kuongoza mkutano wa viongozi wa Ulaya kujadili jinsi ya kufikia amani nchini Ukraine, siku mbili tu baada ya ziara ya kihistoria ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, huko Washington DC.