Jumatano , 5th Mar , 2025

Kocha wa Liverpool Arne Slot amesema timu yake haiwezi kuitwa  timu bora zaidi barani Ulaya hadi watakaposhinda Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Arne Slot - Kocha wa Klabu ya Liverpool

The Reds wameongoza hatua ya ligi ya Ligi ya Mabingwa wakiwa wameshinda mechi 7 kati ya 8 na kwa sasa wanaongoza Ligi Kuu ya Uingereza  kwa tofauti ya alama 13, hii leo wako Ufaransa   kupambana na PSG  katika mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora.

"Ni pongezi nzuri kupata lakini timu bora zaidi barani Ulaya inapaswa kushinda Ligi ya Mabingwa lakini sisi tuko mbali na hilo, tunaanza na mchezo mgumu sana  dhidi ya PSG,kwa upande wangu ukiniuliza timu bora nitajibu Madrid ambao wamebeba kombe hili msimu uliopita "

 Arne Slot akijibu kauli ya kocha mkuu wa PSG Luis Enrique aliyesema Liverpool ni timu bora.