Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime, imeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mkoani Dodoma na Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu la Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nikson Idala Jakson.
"Uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata binti aliyefanyiwa ukatili huo na amehifadhiwa eneo salama na anaendelea kupata huduma zinazostahili kupewa mtu aliyefanyiwa ukatili wa aina hiyo, aidha uchunguzi umebaini tukio hilo lilifanyikia eneo la Swaswa katika Jiji la Dodoma mwezi Mei 2024," imeeleza taarifa hiyo.
Aidha DCP Misime amesema kuwa, "Jeshi la Polisi lingependa kueleza pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne huko Dar es Salaam waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo,".