Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema wachezaji watatu, nyanda Aishi Manula, mlinzi Henock Inonga na winga Aubin Kramo watakosekana kwenye huo mchezo.
Wednesday , 27th Sep , 2023
Kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya miamba ya Zambia, Power Dynamos, klabu ya Simba imethibitisha kuwa itawakosa wachezaji watatu kutokana na majeraha.