
''Ingawa ma-paroducer wote na-enjoy kufanya nao kazi, lakini lazima ni mtaje pancho na nikitoka kumtaja pancho lazima nimtaje Allen Mapigo, kwa sababu nilifanya nao Dar es salaam stand up, na Pancho kwa sasa ni marehemu kwahiyo ni lazima niwakumbushe kwamba Dar es salaam stand up kafanya Pancho Latino'' alisema Chid Beenz.
Mbali na Chid Beenz kuwa na mpango wa kuja na ''remix'' ya wimbo wa Dar es salaam stand up amefunguka pia kwa kusema bado yupo kwenye kufahamu ni nani awepo, vilevile wapo baadhi ya mashabiki zake wanaomba usifanyiwe ''remix'' ili kutunza ubora wa wimbo huo.