Friday , 15th Sep , 2023

Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya Abdul Hamid Al-Dabaiba amesitisha masomo nchini kote kwa siku 10, katika kuonyesha mshikamano na Walibya walioathirika na mafuriko ya Septemba 11.

 

Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayotambuliwa kimataifa nchini Libya, ambayo iko katika mji mkuu Tripoli, ilitoa tangazo hilo jana jioni.

Serikali mbili hasimu nchini Libya, serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa kimataifa inayoongozwa na waziri mkuu Al-Dabaiba na serikali ya mashariki mwa Libya, inayoongozwa na waziri mkuu Osama Hamad, zote zimekuwa zikifanya juhudi za kukabiliana na mafuriko mashariki mwa Libya.

Tangazo hilo limeongeza kuwa kusitishwa kwa masomo kutaruhusu shule kutumika kama makazi ya muda kwa waathirika wa mafuriko.

Kuna hofu kwamba watu 20,000 huenda wamekufa kutokana na mafuriko makubwa yaliyolikumba eneo la mashariki mwa Libya siku ya Jumapili.

Meya wa mji wa bandari ulioharibiwa wa Derna alisema idadi hiyo ilitokana na idadi ya wilaya zilizoharibiwa kabisa wakati mabwawa mawili yalipopasuka, na kutoa tsunami ya maji wakati watu wamelala.

Zaidi ya watu 5,300 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 30,000 wameachwa bila makao kutokana na mafuriko makubwa