Wednesday , 13th Sep , 2023

Vyumba viwili vya madarasa na madaftari ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Iyela Jijini Mbeya, vimeteketea kwa moto huku chanzo chake halisi bado hakijafamika.

Akizungumza na EATV Kamanda wa Zimamoto na Ukoaji Mkoa wa Mbeya Malumbo Mgata, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema chanzo bado hakijajulikana huku akitoa wito kwa wananchi kutunza wa mali za umma.

"Madhara ni kuungua kwa madarasa mawili ambayo ndiyo ilikuwa yakitumiwa kuifadhia vifaa vya wanafunzi chanzo mpaka sasa hakijabaini nini na uchungzi kwa kina unaendelea" - Malumbo  Mgata, Kamanda Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.

"Nimepigiwa simu saa moja na nusu  kwamba balozi wai huku madarsa yanaungu ndipo nikachukua hatu ya kupiga filimbi na vuvuzela baada kufika na kuona hali si nzuri ndipo wananchi wamekuja kwa wingi" Balozi  wa mtaa Charles Hoza Mtaa Iyela moja

Issa Mohamed Njechele ni Mwenyekiti  Serikali ya mtaa Iyela Moja kata ya Iyela jijini Mbeya amezungumzia ajali hiyo huku mkuu Mkuu wa Shule Sekondari ya Iyela Mwalimu Stephano Kamendu, na Mwalimu Devetho Hoza wakieleza kuwa moto huo umechomwa  na mmoja wawafunzi wa shule hiyo.

"Tumefanya jitihada kubwa sana kuzima moto faya nao wakawa wamefika  tukaendelea kkuzioma na tunashukuru mungu hakuna madhara kwa binadamu" Issa Mohamed Njechele, Mwenyekiti Mtaa wa Iyela moja

"Kimsingi  nimehamia hapa mwaka jana kilikuwa ndo kituo cha wavuta bangi lakini tukapambana mpaka ninapo zungumza dakika hii hakuna mwanafunzi anaye vuta bangi" Stephano Kamendu Mkuu wa Shule sekondari Iyela 

"Inavyosemekana kwamba  kuna mtoto amekuja kutupia moto humu wa sekondari hapahapa maana mtoto wa praymary amesema kuwa amemuona mkaka moja aamerusha mpoto hapa amekimbia hapa enepo la shule alivyotupia moto akapotea" alisema mwalimu Devetha Hoza