Tuesday , 5th Sep , 2023

Simon Charles Mkazi wa Masanga Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma, anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 32, amefariki Dunia baada ya kuporomokewa na Jiwe wakati akichimba Madini Ujenzi katika Mgodi wa wachimbaji wadogo uliopo eneo la Masanga Mjini Kigoma

Mwenyekiti wa wachimbaji Wadogo katika Mgodi wa Masanga Khassan Khamimu, amesema licha ya kuwa wanachukua tahadhali bado mazingira hayako salama kwa wachimbaji

Afisa Mtendaji Kata ya Gungu Mwanvita Rusovu ameshauri wachimbaji hao kusitisha shughuli hadi mazingira ya uchimbaji yatakapo kuwa salama kuepusha Matukio ya kuporomokewa na mawe.