
Uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi ulikamilika kwa Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi.
Wanajeshi 12 wameonekana kwenye televisheni wakitangaza kuwa wanafuta matokeo ya uchaguzi na kuvunja taasisi zote za jamhuri hiyo.
"Tumeamua kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo, utawala usiowajibika, usiotabirika na kusababisha kuzorota kwa uwiano wa kijamii ambao unahatarisha nchi katika machafuko" amenukuliwa mwanajeshi mmoja katika tamko hilo