Saturday , 1st Jul , 2023

Mkataba wa mradi ujenzi wa mabasi yaendayo haraka (DART) awamu ya nne kutoka katikati ya mji hadi Tegeta umesainiwa Dar es Salaam huku serikali ikisisitiza ujenzi wa miradi kujengwa kulingana na thamani ya fedha.

Hayo yamebainishwa katika hafla ya utiaji saini wa mikataba minne ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa haraka wa mabari (BRT) awamu ya nne Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na Mradi wa ujenzi wa Barabara Mkoa wa Pwani, ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya huku akisisitiza na wakandarasi wazawa kuchangamkia fursa za tenda za ukandarasi. 

Aidha Mhandisi Kasekenya amefafanua kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwenye miradi ya awamu zilizopita ili mapungufu hayo yasijitokeze kwenye ujenzi wa awamu hii na awamu zijazo.

Mbali na kupongeza nia ya serikali kwenye maboresho ya miundombinu Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima akaiomba Serikali kuwasaidia ujenzi wa mitaro ya maji taka itakayosaidia kupunguza mafuriko katika jimbo la Kawe ambayo yamekiwa yakisababisha uharibifu wa vitu na vifo vya watu.