Wednesday , 28th Jun , 2023

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata muuzaji sugu wa bangi aitwaye Maneno Bundala (28), mkazi wa Majimatitu, Mbagala na wenzake wawili wakiwa na bangi gunia saba 7, puli 445, mbegu za bangi kg 5 na magazeti ya kufungia bangi wakiwa wameyaficha kwenye nyumba yao.

Bangi

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 28, 2023, na Kamanda wa Polisi Knda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro

Aidha katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa sugu 48 wa matukio ya unyang’anyi na uvunjaji nyumba usiku na kuiba huku likitoa onyo kali kwa watu ambao wamekuwa wakinunua bidhaa zinazoibwa mtaani.

Miongoni mwa waliokamatwa kuwa ni Michael Jacob ngatunga (38) mkazi wa Jet lumo, Hossein Rashid (40) Mkazi wa Mtoni Mtongani na Mussa Mohamedi (23) mkazi wa Chanika, wote wa Dar es Salaam.