Tuesday , 6th Jun , 2023

Jengo la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Shinyanga limeteketea kwa moto na kuunguza maduka saba yaliyokuwa kwenye jengo hilo pamoja na mali zilizokuwa ndani huku maduka sita yakinusurika

Moto huo ambao unadaiwa kuanza kuwaka majira ya saa tisa usiku katika jengo hilo ambalo lina jumla ya maduka 13 na kuunguza maduka saba na mali zote zilizokuwa ndani

Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala amesema jengo hilo lilikuwa ni kitega uchumi kwenye jumuiya hiyo,huku akiwapa pole wafanyabiashara ambao mali zao zimeungua.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Martin Nyambala amesema wamefika eneo la tukio na kukuta moto umeshaunguza sehemu kubwa ya jengo hilo.