
Wakizungumza na #EARADIO familia hizo zimesema hali hiyo imewasababishia kushindwa kutoka kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi na hivyo kutumia muda mwingi kuchota maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao na kuyamwaga nje huku wakieleza vyombo pamoja na vitanda vimesombwa na maji
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Mkunguni A Jumanne Said ameiomba serikali kuharakisha zoezi la kuwalipa fidia wananchi hao kwani walishafanyiwa tathimini na kutakiwa kuondoka