Tuesday , 30th May , 2023

Licha ya serikali kuweka juhudi za kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya kumeibuka tabia ya kuchanganya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi kwenye vyakula kama vile biskuti, asali, juisi, majani ya chai na keki.

Bangi

Hayo yamebainishwa leo Mei 30, 2023, Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera ,Bunge na Uratibu Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini ya mwaka 2022.

Amesema taarifa ya Dunia ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2022 inainyesha kuwa asilimia 40 ya nchi zenye matumizi makubwa ya bangi, zilikumbwa na idadi kubwa ya magonjwa ya afya ya akili, uhalifu na uvunjifu wa amani yaliyosababishwa na matumizi ya dawa hizo.