Saturday , 4th Feb , 2023

Ajali ya gari iliyotokea eneo la Magira Gereza, Mombo Wilayani Korogwe majira ya saa 4:30 usiku wa kuamkia leo, imesababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 12. 

Muonekano wa gari aina ya Coaster baada ya kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso

Ajali hiyo iliyohusisha magali mawili ambayo ni gari namba T.673 CUC aina Mitsubish Fuso iligongana na gari namba T.863 DXN Bus aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.

 Magari mawili aina ya Coaster na lori aina ya Mitsubishi Fuso baada ya kugongana

Mkuu wa Mkoa Wa Tanga Omary Mgumba amesema, chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa  gari Mistubish Fuso kulipita gali la mbele yake bila ya kuchukua tahadhari kulikosababisha kugongana uso kwa uso na Coaster.

Lori aina ya Mitsubishi Fuso baada ya kugongana na Coaster 

Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospital ya Mkoa wa Tanga Bombo na majeruhi wawili wamesalia katika Hospital ya wilaya ya Korogwe kwa matibabu. 

Tukio la ajali baada ya kukaguliwa na polisi akiwemo RTO, magari yote yameshaondolewa barabarani kuruhusu   barabara iendelee kupitika.

Tazama sehemu ya kipande cha video kwenye ajali hiyo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali hiyo.