Monday , 28th Nov , 2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameeleza kuridhishwa na Ujenzi wa Dajara la Mbuchi lililopo kibiti Mkoani pwani huku akiipongeza TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri ya Usimamizi na Ujenzi wa Daraja hilo

Ameeleza kuwa Ujenzi wa Daraja hilo ni dhamira ya Serikali ya Kuhakisha inawafikia Wanchi mpaka Vijijini Hivyo ndiyo maana Serikali imeanzisha Wakala wa Serikali wa Barabara Vijijini TARURA ili kumaliza changamoto za barabara kwa wananchi

Aidha Waziri Mkuu amemwagiza Waziri TAMISEMI  Kushughulikia Ujenzi wa Barabara Unganishi inayotokea  Mhoro mpaka Mbuchi.

Waziri mkuu Majaliwa amewataka Wananchi kuchangamkia Fursa za Kiuchumi zilizopo katika eneo hilo ili kuweza kujipatia kipato kitachonufaisha familia zao. 

Katika hatua Nyingine Mhe. Majaliwa amewataka Wafugaji kufuga kulingana na Maeneo wanayoyamiliki.
Ameelekeza Serikali za Vijiji zitambue Mifugo yote iliyopo na Maeneo yao na Viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya kusimamia kila Mfugaji awe na eneo la kufugia.

Waziri Mkuu Majaliwa amekemea Tabia ya mapigano ya Wakulima na Wafugaji na kutaka wachukuliwe hatua kwa mfugaji ambaye hathamini maisha ya wengine.

Aidha Mhe Majaliwa ameitaka Halmashauri hiyo kujenga Zahanati kila kijiji kupitia fedha za ndani.
Amesisitiza Utunzaji wa Misitu ya Mikoko na kutaka Wananchi wa Mbuchi kutafuta chanzo kingine cha mapato na Biashara kwa Ukataji wa Miti huo utathiri  Mazingira na vyanzo vya Maji.

Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaji Aboubakar Kunenge amesema kuwa eneo la Mbuchi ni eneo la Kimkakati kwa Uchumi wa Mkoa kwani kuna shughuli kubwa za Kilimo na Uvuvi zinazofanywa na wananchi kwa ajili ya kujiongezea kipato na uchangiaji wa pato la taifa kupitia kodi mbalimbali. 

Kunenge ameshukuru Rais ambae amekua akifanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi bila ubaguzi kwa kuhakikisha anatatua changamoto walizonazo.