Sunday , 20th Nov , 2022

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema mbali na ukarabati wa uwanja huo, Serikali pia ina mpango wa kujenga uwanja mwingine.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete

Wakati Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ikisema uwanja wa ndege wa Bukoba uko salama, Serikali imekiri kuna changamoto, hasa wakati wa mvua, hivyo kuanza mikakati ya ujenzi wa uwanja mpya mkoani humo.

Suala la kuboresha Uwanja wa Ndege Bukoba, Serikali ina mpango wa kujenga kiwanja kipya Omukajunguti, eneo ambalo lipo uelekeo kama unakwenda Uganda, tayari tumeanza kutafuta fedha Sh9 bilioni kuwalipa wananchi fidia kwa sababu tayari uthamini ulifanyika muda mrefu, japo unatakiwa kurudiwa tena,

Kauli ya Serikali imekuja zikiwa zimepita wiki mbili tangu ilipotokea ajali ya ndege aina ya ATR 42-500 mali ya Precision Air iliyokuwa imebeba watu 43 kutumbukia katika Ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19, huku 24 wakinusurika.

Ajali hiyo illiterate wakati ndege hiyo ikijaribu kutua uwanjani hapo huku ukiwa na hali mbaya ya hewa kutokana na mvua.