Tuesday , 7th Jun , 2016

Waandishi wa Habari nchini Tanzania wametakiwa kutumia taaluma yao vizuri katika kutumia vivutio vya utalii, vilivyomo nchini kwa kuwa ongezeko la watalii litasaidia kuinua uchumi wa Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.

Akifungua kikao cha waandishi na wahariri waandamizi Mjini Morogoro, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, amesema kuwa hakuna nchi ambayo watalii wanaingia kwa wingi bila kupata habari nzuri za vivutio vya utalii vya nchi hiyo.

Prof. Maghembe amesema Tanzania ni nchi ya pili duniani baada ya Brazil kuwa na vivutio vingi, na vyenye viwango lakini kuna changamoto nyingi zinazozikabili sekta hiyo ikiwemo kutokupata kutangazwa vizuri kutoka kwa wanahabari nchini.

Aidha, amesema kuwa Chagamoto nyingi ni pamoja na hifadhi nyingi kuvamiwa na wafugaji huku sheria za uvamizi wa hifadhi zikiwa hazifuatwi ikiwa ni pamoja na kuwakaguwa wafugaji wanaohama na makundi makubwa ya mifugo ambapo wengi husambaza magonjwa ya mifugo katika hifadhi na kukausha vyanzo vya maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa, Dkt. Allan Kijazi, amesema waandishi wananafasi kubwa ya kuwafichua wahalifu wa maliasili za serikali ikiwemo kuwafichua majangili katika mbuga za Wanyama.

Sauti ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe,