Wednesday , 29th Jun , 2016

Waislam wa dhehebu la Shia nchini Tanzania wameviomba vyombo vya usalama vya kimataifa kuhakikisha vinaweka juhudi za dhati katika kuumaliza mgogoro unaoendelea kati ya Palestina na Israel kwani wananchi wa nchi hizo wanapata mateso makubwa.

Akiongea leo Kiongozi Mkuu wa Waislam wa dhehebu la Shia Ithna Sheriya nchini Tanzania, Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa mgogoro unaoendelea katika nchi hizo mbili unaweza sababisha machafuko katika nchi nyingine endapo hautatafutiwa ufumbuzi kwani kuna viashiria kuwa migogoro inayoendelea katika nchi nyingine chanzo chake ni Palestina na Israel.

Julai mosi Waislam wa Shia wanaadhimisha siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ni jina la msikiti uliopo nchini Palestina hivyo waumini hao nchini Tanzania wameamua kusheherekea kwa kupaza sauti zao kuhamasisha amani nchini Palestina ili Dunia nzima iendelee kuwa na amani.