Sunday , 2nd Oct , 2022

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima, amewaomba wazee kubadilisha hadithi za kale walizo wasimulia wajukuu zao kuhusiana na Imani za kishirikina na badala yake wakawahadithie hadithi zitakazowajenga na kuwa raia wema kwa taifa.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo leo Oktoba 02, 2022 wakati wa Kongamano la Wazee kuelekea Kilele cha Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
 
Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, zipo baadhi ya Jamii, wakiona mzee macho yamekuwa mekundu na yanatoa Machozi na wengine wamezeeka na Migongo kupinda huibuka na dhana kuwa ni washirkina jambo ambalo sio la kweli hivyo nilazima tubadili fikra hizo kwa sasa.
 
"Wazee wangu niwaombe sana, kama kuna baadhi yenu waliwahi kuwahadithia wajukuu juu ya Habari za kishirikina huko nyuma na kuchochea Vitendo vya Ukatili basi ni wakati wa kuwabadili Fikra kwa kuwapa hadithi zitakazo wafanya kuwa Raia wema kwa Taifa lao" alisema Dkt. Gwajima