Bw. Zuma alijiuzulu kwa tuhuma za rushwa ambazo anakana mpaka sasa. Amesema kwamba siku ya jumatatu alifuatwa na baadhi ya wananchama wa chama tawala nchini humo cha ANC , wakimtaka awe mwenyekiti wa chama hicho , ikiwa ni kuelekea mkutano wake mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu.
Amesema kwamba hawezi kukataa wito huo endapo watamuhitaji kuja kukitumikia chama hicho kwa mara nyingine katika ufanisi.
Ameongeza kuwa chama cha ANC kinapitia changamoto za umoja .