Taasisi ya Mifupa MOI
Mkurugenzi wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahanu MOI Dkt Laurent Mchome, amesema ugonjwa wa kupooza unaoongoza kwa kuwapata wananchi hasa wenye umri wa kuanzia miaka 40 ni damu kumwagikia ndani ya ubongo kutokana na mifumo ya mishipa ya damu kushindwa kupitisha damu kutokana na mafuta mengi mwilini.
Amesema kama Watanzania hawatabadilisha aina ya maisha ikiwemo ulaji wa vyakula visivyo na uhai kwenye mwili tatizo hilo la watu kupooza mwili litaendelea kuwa kubwa na taasisi hiyo inaweza ikazidiwa na wagonjwa wa aina hiyo