Kamanda wa Polisi Katavi Ali Hamad Makame, amesema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi waliandaa msako mkali wa kupambana na uhalifu na waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na pikipiki ya wizi yenye Namba za usajiri MC 915 CDV aina ya HONLG yenye rangi nyekundu.
Kamanda Makame amesema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufanyiwa mahojiano ya kina amekiri kuwa aliiba pikipiki nyingine nne kwenye maeneo tofauti tofauti ya Mkoa wa Katavi na aliweza kwenda kuzionesha pikipiki hizo.
Makame ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiiba kwa kutumia mbinu ya kutembea na funguo bandia ambazo ndizo alikuwa akizitumia kuibia pikipiki zinazokuwa zimepakiwa kwenye maeneo mbalimbali na wamiliki wa pikipiki hizo.